NAAMINI HII BLOG ITATUWEKA KARIBU WANA NDUGU TULIO WENGI AMBAO TUKO MAENEO MBALIMBALI DUNIANI,ZAIDI WALE WALIO CHINI YA KIZAZI CHA MZEE LANG'O NA KUFAHAMIANA ZAIDI
Mimi naitwa Naftali Kwang’a John Adhero. Nilizaliwa siku ya Alhamisi tarehe 23 Machi, 1944 katika familia ya Mzee Yohana (John) Adhero Lang’o na mama Rebeka Ogembo Adhero, nikiwa ni mtoto wa pili kwa mama kati ya watoto kumi na mbili waliozaliwa katika familia hii – wavulana watano na wasichana watano. Nilipewa jina la Kwang’a – jina la Mzee maarufu katika ukoo wetu – likiwa na maana ya ‘nivushe’ ng’ambo ya mto au ziwa.
Nilizaliwa katika kijiji cha Kowak, kata ya Nyathorogo, Tarafa ya Luo- Imbo, Wilaya ya North Mara (baadaye Tarime) na hivi karibuni Rorya. Kabila langu ni Mluo – moja ya makabila yaliyoishi kando kando ya mto Nile. Na ndiyo sababu kabila hili linaitwa Nilotic – na limetapakaa Sudan ya Kusini, Ugana ya Kaskazini, Mashariki ya Ziwa Victoria huko Kenya na Wilaya za Tarime na Rorya Mkoani Mara hapa Tanzania.
NAAMINI HII BLOG ITATUWEKA KARIBU WANA NDUGU TULIO WENGI AMBAO TUKO MAENEO MBALIMBALI DUNIANI,ZAIDI WALE WALIO CHINI YA KIZAZI CHA MZEE LANG'O NA KUFAHAMIANA ZAIDI
ReplyDeleteNawapongeza kwa kuanzisha hii blog kwani itawaleta ndugu, jamaa na marafiki kuwa pamoja, vilevile kubadilishana mawazo hasa kwa wale walio nje ya Tz.
ReplyDelete